Friday 2 March 2018

MRADI MKUBWA WA JENGO LA HALMASHAURI YA WILAYA YA KILOMBERO WAENDELEA



Katika kurahisisha na kuboresha utoaji huduma kwa wananchi wake, Halmashauri ya wilaya ya Kilombero imeamua kujenga jengo hilo ambalo ‘contractor’ wake ni GROSS INVESTMENT LTD. Jengo hilo litakalokuwa lina kila Idara na lenye weledi wa hali ya juu kimuonekano.
Jengo hili lenye ghorofa mbili na ambalo ndilo linaweza kuwa jengo kubwa na la kisasa kabisa kwa halmashauri zote nchini Tanzania linajengwa pembeni kidogo mwa jengo ambalo linatumika kwa sasa kutolea huduma za ki halmashauri.
Aidha jengo hilo litakapokwisha litakuwa na uwezo wa kuchukua Idara zote pamoja na kufanyia shughuli zote zinazotakiwa kufanywa na Halmashauri ya manispaa ya Kilombero.
Kwa sasa wafanyakazi wa Halmashauri ya wilaya ya Kilombero wana ari kubwa sana ya kukamilika kwa jengo hilo kwani litakuwa msaada mkubwa sana wa utendekaji wa kazi kwa weledi na ufanisi wa hali ya juu ukilinganisha na ufanisi mkubwa unaofanywa kwa sasa, utatoa nafasi za kutosha kuhakikisha kila kitu kinakwenda sawa.
KARIBUNI SANA KILOMBERO

No comments:

Post a Comment