Friday 2 March 2018

TAARIFA YA MAENDELEO YA KILIMO KATIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA KILOMBERO 2018Kwa mujibu wa Afisa Kilimo wa Halmashauri ya wilaya ya Kilombero ndugu Mohammed Ramadhani juu pichani aliyesimama, ifuatayo ni taarifa fupi ya hali ya kilimo katika halmashauri ya wilaya ya kilombero 
kama alivyoongea na Afisa habari wa Halmashauru hiyo ndugu ISLAM MPOSSO
1.0 Hali ya chakula Wilaya ya Kilombero Feb 2018
Kwa mujibu wa Sensa ya watu  na makazi 2012 Wilaya ya Kilombero ina wakazi wapatao 407,880 na jumla ya kaya 94,604. Ongezeko la idadi ya watu kwa mwaka ni asilimia 2.4, hivyo kadirio la idadi ya watu kwa mwaka 2016/17 ni Halmashauri ya Wilaya kuwa na watu 344,410. Mahitaji halisi ya chakula mchanganyiko kwa mwaka itakuwa ni tani 138,194 (tani 124,374.6 za chakula aina ya wanga na tani 13,819.4 za chakula aina ya utomwili).   Utekelezaji wa malengo/uzalishaji 2016/17 ni tani 572,664 hivyo  ikiwa ni ziada ya tani 434,470.Hivyo Halmashauri ina chakula cha kutosha na hakuna tishio la njaa katika ujumla wake.
1.1. Upatikanaji wa Chakula na Bei zake 
Upatikanaji wa chakula ni mzuri kwa ujumla, isipokuwa bei ya baadhi ya vyakula hasa mchele imepanda katika kipindi hiki kwa sababu baadhi ya maeneo mengi ya nchi hayakuzalisha chakula cha kutosha. Hali hii imesababisha wanunuzi kutoka maeneo mbalimbali ya nchi kuja kununua mchele kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero lakini hali iko tofauti katika zao la mahindi bei imeendelea kupungua hadi kufikia Tsh.10,000 kwa debe kwa bei ya juu na chini ni 5,500. Tazama jedwali No.1 hapo chini:-
Jedwali Na.1: Bei ya Mazao Sokoni.

NaAina ya ChakulaUpatikanaji wa
Chakula Sokoni
KinakopatikanaBei ya
chini kwa 
kilo/Tsh.
Bei ya 
juu kwa 
kilo/Tsh.
Kinapatikana/
Hakipatikani
Ndani ya
wilaya
Nje ya 
Wilaya
1MahindiKinapatikana
306556
2MpungaKinapatikana 533867
3NganoKinapatikana
2,0002,500
4MtamaKinapatikana1,8002,000
5UleziKinapatikana
1,5002,500
6UweleKinapatikana
2,0002,500
7MakopaKinapatikana1,6002,200
8Mhogo mbichiKinapatikana
6501,150
9Viazi vitamuKinapatikana9501,150
10Viazi MviringoKinapatikana
1,0001,250
11NdiziKinapatikana
8501,050
12MaharageKinapatikana
1,8002,400
13Mikunde mingineKinapatikana1,5001,800

Nb. Mchele bei ya chini ni Tsh.1,450 na ya juu ni 2,000 kwa kilo.
      Unga wa Mahindi bei ya chini ni Tsh. 1,000 na ya juu ni 1,250 kwa kilo.
Halmashauri ya Wilaya inaendelea kuhamasisha Wananchi kuwa na tabia ya kuhifadhi chakula cha kutosha kwa ajili ya matumizi ya mwaka mzima kwa:-
Kutoa elimu ya matumizi sahihi ya chakula.
Kupanua wigo wa kulima mazao mengine badala ya chakula badala ya kutegemea zaidi zao la mpunga.
Kuhimiza wananchi kupanda mazao yanayokomaa kwa muda mfupi na yanayostahimili ukame.
-Kuhimiza wakulima walioko katika maeneo ya umwagiliaji kuendelea kuzalisha zaidi ya mara moja kwa mbinu ya mazao mchanganyiko pale inapoonekana maji hayatoshelezi kulima mpunga eneo lote.
1.2. Hali ya Hewa
 Kwa msimu 2017/18 mvua zimeanza kunyesha kwa muda muafaka, japo hazina matawanyiko mzuri lakini tayari kazi muhimu za maandalizi ya mashamba, upandaji na utunzaji wa mimea iliyopo shambani unaendelea. Katika mwezi Februari kumekuwa na upungufu mkubwa wa mvua kulikopelekea baadhi ya maeneo yaliyopandwa zao la Mahindi kuathirika kwa kukosa unyevu wa kutosha kuzalisha. Tazama jedwali Na.2. linaloonesha mwanguko wa Mvua kwa kituo kilichopo bomani;-

Jedwali Na.2 Mwanguko wa Mvua - Msimu 2017/2018 hadi Feb 25 2018
MweziSeptOctobaNovDisembaJanuariFebruari
Jumla mm.
0
0
49.8
137.9
261.4
2.7
Idadi ya Siku
0
0
6
5
9
1
2.0.    Hali ya Uzalishaji wa Mazao ya Chakula
Utekezezaji wa malengo ya Kilimo kwa mwaka umekuwa ukiathiriwa sana na mabadiliko ya hali ya hewa hasa mvua ambazo zimekuwa si zauhakika wa kutosheleza mahitaji ya unyevu kwa mazao yaliyopo shambani. Mvua hizi ama  huchelewa kuanza kunyesha na kusababisha kuchelewa kupanda mazao mashambani na kusababisha mazao kutokomaa vizuri, au zinanyesha nyingi na kuathiri maandalizi ya mashamba, upandaji na mazao yaliyopo shambani.
Yafuatayo ni majedwali yanayoonesha hali halisi ya uzalishaji wa mazao ya chakula katika msimu 2016/2017 pamoja na Utekelezaji na matarajio ya mavuno msimu wa mwaka 2017/18  hadi Jan. 2018:- 

Jedwali No.3. Utekelezaji wa Malengo Msimu 2016/17
UTEKELEZAJI WA MALENGO YA KILIMO MSIMU 2016/17
ZaoMalengo kwa mwakaUtekelezaji 
Mazao ya ChakulaEneo litakalopandwa (ha)Matarajio ya mavuno (tani)Eneo liliopandwa (ha)Mavuno Halisi (tani)
Mahindi
38,202
95,505
27,885
69,713
Mpunga
108,865
381,027
101,056
353,696
Mtama
629
629
248.6
284.9
Uwele
0
0
0
0
Ulezi
7
4.2
6
6
Mihogo
9,572
191,440
1780
35600
Viazi vitamu
5,873
70,470
2041.6
24417.2
Ndizi mbivu
2,630
78,912
840.2
24346
Ndizi mbichi
4,678
131,880
2168
64130
Kunde
1,657
1,326
415
319.9
Maharage
217
195
152
150.8
Jumla Ndogo
172,330
951,388
136,592
572,664
 Mazao ya BiasharaMiwa
5,909
472,744
5444.7
277420
Alizeti
912
1,368
24.8
37.3
Ufuta
10,145
10,145
3093.9
3145.5
Kakao
3,112
3,112
1462
1462
Nazi
1,919
13,435
1215.3
8555.1
Jumla Ndogo
21,997
500,804
11,241
290,620

Mazao MengineEmbe
1,457
21,851
984
12,735
Chungwa
617
9,260
275.9
3,602
Tikiti maji
1,339
26,780
280.4
6,617
Vitunguu
391
7,814
10.4
183
Bamia
796
7,964
125.9
1,240
Nyanya
1,875
16,405
186.5
1,637
Nyanya chungu
1,199
8,994
237
1,807
Chinees Cabbage
847
10,585
142.7
1,812
Jumla Ndogo
8,521
109,653
2,242
29,632
Jumla Kuu
202,848
1,561,845
150,076
892,915


Jedwali No.5.  Malengo ya Msimu 2017/18
MALENGO YA KILIMO NA UTEKELEZAJI MSIMU 2017/18
ZaoMalengo kwa mwakaUtekelezaji hadi Jan.2018
Mazao ya ChakulaEneo litakalopandwa (ha)Matarajio ya mavuno (tani)Eneo liliopandwa (ha)Mavuno Halisi (tani)
Mahindi
28,775
76,793
14,807.2

Mpunga
104,078
371,689
63,945.8

Mtama
1275.4
2353.3
33

Uwele
2
3
0

Ulezi
15
20.5
9.5

Mihogo
6,298
125,954
585.1

Viazi vitamu
4,719
56,599
760.4

Ndizi mbivu
2,436
71,464
1,837.2

Ndizi mbichi
5,306
156,883
4,196

Kunde
2,251
1,700
288.8

Maharage
228
280.8
122

Jumla Ndogo
155,383
863,740
86,585
0
 Mazao ya BiasharaMiwa
4,029
201,450
3,461.1
Alizeti
1071.6
1,576
8.5
Ufuta
5,726
5,726
796
Kakao
4,691
4,668
595.7
Nazi
904
6,338
563.6
Jumla Ndogo
16,421
219,758
5,424.9
0

Mazao MengineEmbe
1,083
16,181
960.5
Chungwa
312.6
4,699
211.2
Tikiti maji
488
9,246
161.1
Vitunguu
86.1
1,722
16.5
Bamia
290.9
2,909
160.4
Nyanya
456
4,009
144.8
Nyanya chungu
491
3,681
233.5
Chinese Cabbage
446.9
5,586
139.7
Jumla Ndogo
3,654
48,033
2,011.2
0
Jumla Kuu
175,458
1,131,530
94,021.1
0

3.0.    Changamoto za Uzalishaji wa Mazao.
  • Visumbufu vya mazao hasa panya waharibifu wa mazao(imesababisha baadhi ya wakulima kushindwa kupanda mazao wakisubiri tatizo hilo kupungua) na viwavi vamizi (Fall Army Worms).
  • Kutokamilika kwa miundombinu ya umwagiliaji.
  • Tabia ya wakulima wengi kupendelea kulima zao moja yaani mpunga na kutoyapa kipaumbele mazao mbadala kama Mihogo, Viazi na Ndizi.
  • Kuainishwa kwa mipaka ya Hifadhi ya Bonde la Kilombero kumepunguza maeneo ya kilimo cha mpunga.
  • Mvua tata (Unyeshaji wa mvua mfululizo) Umeathiri shughuli za kilimo kuanzia katika maandalizi ya mashamba na upandaji hasa wa zao la mpunga kutokana na maeneo ya mashamba yaliyoandaliwa kujaa maji.
  • Upatikanaji hafifu wa pembejeo za kilimo hasa mbolea za kukuzia mazao.
  
3.1. Udhibiti wa Visumbufu vya Mazao
  • elimu imeendelea kutolewa namna ya utambuzi na udhibiti wa panya na viwavi jeshi vamizi.
  • Halmashauri imefanya jitihada za makusudi za kununua sumu ya kudhibiti panya(Zinc phoshide) kilo 50 pamoja na kilo 3 salio la msimu uliopita na kusambazwa kwa wakulima na kufanikiwa kuokoa ha.1073.5 za mazao ya nafaka zilizokuwa hatarini kuharibiwa.
  • Kwa kuwa tatizo bado linaendelea Halmashauri kwa fedha za ndani imeshanunua tena sumu kilo 200 kwa ajili ya kufanya kampeni ya kudhibiti panya katika vijiji vyote vilivyoathirika. Kazi hiyo inaweza kuanza rasmi ndani ya wiki hii.